Trump Asema Marekani Itaiweka Venezuela Chini ya Usimamizi wa Mpito

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema kwamba nchi yake itaiendesha Venezuela kwa kipindi cha mpito hadi itakapohakikisha kuna uhamisho wa madaraka ulio salama, sahihi na wa busara, kufuatia operesheni ya kijeshi iliyosababisha kukamatwa kwa Rais Nicolás Maduro na mkewe Cilia Flores.
Akizungumza jana Jan. 3, 2026 katika mkutano na waandishi wa habari akiwa Mar-a-Lago, Florida, Trump alisema hatua hiyo ni muhimu ili kuunda mazingira ya amani, uhuru na haki kwa wananchi wa Venezuela. Aliongeza kwamba nchi hiyo haitarudi mikononi mwa mtu yeyote ambaye hakuangalia maslahi ya watu wa Venezuela.
Kwa mujibu wa Trump, Marekani itaweka ulinzi na usimamizi wa kisiasa wa Venezuela hadi pale itakapoweza kukabidhi madaraka kwa serikali mpya kwa njia salama na yenye
Trump pia alisisitiza kuwa hakuna mwanajeshi wa Marekani aliyeuawa wala vifaa vya kijeshi kuteketea wakati wa operesheni hiyo. Alidai kuwa Maduro na mkewe watashtakiwa na kuhukumiwa chini ya sheria za Marekani kutokana na tuhuma zinazohusiana na usafirishaji wa dawa za kulevya.
Halikadhalika, Trump alisema kwamba Jamuhuri ya Venezuela itakuwa chini ya usimamizi wa Marekani hadi pale itakapopatikana hali ya kisiasa imara kwa ajili ya uhamisho wa madaraka.

