The House of Favourite Newspapers
gunners X

Video: Mke wa Saidi Fella azungumzia hali ya mumewe na sapoti anayoipata

0

Mke wa Saidi Fella, Sweet Fella amesema kuugua kwa mumewe kwake ni ibada.

Sweet ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba yupo pamoja sana na mume wake huyo mpaka dakika za mwisho.

Akielezea kwa kina kuhusu kuugua kwa mumewe Fella na mambo yanayojitokeza, Sweet aliandika:

“Leo hii hakuna mtu yeyote anayekuulizia hali yako lakini mimi najua mambo yote uliyowafanyia watu nao wanajua yote ila ‘wanajizima data’.

“Wote uliowasaidia na wanaonisapot (kipindi hiki kigumu) nawatambua, inshallah Mungu atawalipa kwa hicho mnachojitolea, Mungu awasaidie. Namuombea mume wangu apone atakuja kuongea mwenyewe yote.

“Kwa kifupi simfagilii mtu yeyote, nitapambana pamoja na watu wanaonisapoti. Nitakuja kuwashukuru baadaye na nitakuja kuwataja kwa majina,” alimalizia Sweet, mke wa Fella.

Baada ya kuuona ujumbe huo, Global TV ikamtafuta na kuzungumza naye kuhusu alichokiandika na kuhusu hali ya mumewe.

Leave A Reply