
Klabu ya Chelsea imethibitisha uteuzi wa Liam James Rosenior kuwa kocha mkuu mpya, akichukua nafasi ya Enzo Maresca aliyefutwa kazi wiki iliyopita.
Rosenior, mwenye umri wa miaka 41 na raia wa England, alikuwa akiinua Strasbourg — klabu inayomilikiwa na kampuni ya BlueCo, ambayo pia ni wamiliki wa Chelsea. Ameingia mkataba wa miaka sita na nusu ambao utamuweka Stamford Bridge hadi Juni 2032.

