Access Microfinance Bank Sasa Kutambulika Kwa Jina Selcom Microfinance Bank
Tunayofuraha kutangaza hatua muhimu katika safari yetu ya kuelekea kukuhudumia vyema, Benki ya Access Microfinance Tanzania Limited inaendelea kukua, kuimarika na kuja na mabadiliko makubwa chanya. Kuanzia tarehe Juni 4, 2024, tutafanya kazi kwa fahari kuu chini ya jina jipya, Selcom Microfinance Bank Tanzania Limited. Ubadilishaji chapa huu unaonyesha dhamira yetu ya kubadilika kulingana na mahitaji ya wateja wetu na kujielekeza kwetu kutoa huduma zilizo sahihi zaidi na fasaha za kifedha zilizojaa ubunifu mkubwa.
Selcom Paytech Limited, mwanahisa wetu mkubwa, anabeba jina linaloaminika katika tasnia ya huduma za kifedha na malipo kwa zaidi ya miaka 22. Selcom Paytech, ambayo ni maarufu kwa maendeleo na kutegemewa, imekuwa mstari wa mbele katika ubunifu na uvumbuzi nchini. Tunapohamia Selcom Microfinance Bank Tanzania Limited, tunaleta pamoja nasi kiwango kile kile cha ari, kutegemewa, ubunifu na uvumbuzi ambacho umekuwa ukiufurahia na kukidhi matarajio yako.
Kama sehemu ya kuimarisha uonekao wetu, Benki ya Selcom Microfinance Tanzania Limited inaleta utambulisho mpya kwa muonekano wake na rangi kuu za muonekano zikibadilika kuwa nyekundu, nyeupe na nyeusi. Ingawa sura ya nje ya mwonekano wetu inabadilika, ahadi zetu dhabiti kwako ni kutoa huduma zilizoboreshwa zinazozidi matarajio yako na kukufanya uwe nasi daima.
Kutokana na michakato maalum iliyoboreshwa katika utoaji wa huduma zetu zilizoboreshwa kipeee kabisa, tumejitolea kwa dhati kabisa kuboresha uzoefu wako na furaha yako ya huduma za kibenki katika Selcom Microfinance Bank Tanzania Limited kuwa rahisi zaidi, yenye ufanisi na kuridhisha zaidi, kuhakikisha mabadiliko haya kwa wateja wetu yanafanyika kwa urahisi na furaha, bila changamoto, huku vituo vyote vya huduma vikibaki kufanya kazi kwa urahisi kwenye miundombinu iliyo bora na kuongezwa.
“Tunaelewa na kudhamini sana umuhimu wa uaminifu na utegemeo thabiti katika tasnia ya huduma za kifedha, benki yetu itaendelea kutoa ushirikano na kuwa karibu kabisa na wateja wetu kwa kutoa huduma za kifedha kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa, sekta ambayo ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Tanzania”, aliongeza Julius Ruwaichi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Selcom Microfinance Bank Tanzania Limited. Tunapokumbatia utambulisho wetu mpya, lengo letu linasalia katika kudumisha viwango vya juu zaidi vya uadilifu, ubunifu, uvumbuzi na huduma kwa wateja. Tunashukuru kwa kuendelea kutuunga mkono wateja wetu na tunatarajia kuwahudumia chini ya chapa ya Selcom Microfinance Bank Tanzania Limited.
Kwa sheria zinazoongoza nchi yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ieleweke wazi kwamba, mabadiliko haya hayaathiri haki au wajibu wowote wa benki au kutoa kuathiri madai/mashauri yoyote ya kisheria na au dhidi ya wadau wake, wala kanuni, kila kitu kitakuwa kinahama kutoka Access Microfinance Bank Tanzania Limited hadi Selcom Microfinance Bank Tanzania Limited.
Selcom Microfinance Bank Tanzania Limited inatoa shukurani zake za dhati kwa wateja wake wote, washirika, na wadau kwa ushirikiano uliotukuka katika safari hii ya uwekaji chapa mpya.
Kwa taarifa zaidi kuhusu Selcom Microfinance Bank Tanzania Limited na huduma zake, tembelea; Tovuti; www.smfb.co.tz , Nambari ya simu 0659 074 000/ 0746 985 840.
#SelcomInatosha