Khadija Mngwai |CHAMPIONI IJUMAA| Dar es Salaam
MSHAMBULIAJI wa Simba, Ibrahim Ajibu, amefunguka kwa kusema kuwa nia yake ni kujituma kwa nguvu zote kuisaidia timu yake kuchukua ubingwa lakini kuelekea mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar napo ametoa neno.
Kuonyesha kuwa yupo tayari kwa lolote, Ajibu ambaye alipata maumivu alipokuwa akiitumikia Taifa Stars dhidi ya Burundi, Jumanne ya wiki hii na hivyo kulazimika kutoka moja kwa moja uwanjani, amesema yupo tayari kucheza mchezo dhidi ya Kagera hata kama atakuwa na maumivu.
Katika mchezo wa Stars, alitoka akiwa amefungwa bandeji huku akichechemea lakini kuhusu mchezo huo wa keshokutwa Jumapili alisema:
“Kweli nina maumivu lakini kwa kizungu tunaita ni ‘small pain’ hivyo hayawezi kunizuia mimi kucheza dhidi ya Kagera, naamini ndani ya siku mbili tatu nitakuwa vyema na maumivu yatakata na kuweza kuendelea na mchakato wa kusaka ubingwa.
“Tunahitaji kushinda katika michezo yetu yote iliyo mbele yetu kwani tunajituma ipasavyo kuweza kufanikiwa kufanya vyema kwani kila mchezo tutakaocheza utakuwa na ushindani mkubwa, hivyo siyo muda wa kupoteza nafasi.”
Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe nisiasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, muziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.
Comments are closed.