The House of Favourite Newspapers

Aslay Afungukia Matumizi ya Kinga

0

STAA wa Ngoma ya Natamba, Aslay Isihaka, amefunguka kuwa, kwenye maisha yake ya faragha kamwe huwa haachi kutumia kinga kwa ajili ya kulinda afya yake.

Akipiga stori na Over Ze Weekend, Aslay amefunguka kuwa, kutokana na uwepo wa maradhi mbalimbali sanjari na mimba zisizotarajiwa hivyo anahakikisha anatumia kinga kila awapo faragha na mwenzi wake.

“Natumia kinga kila inapobidi, nafahamu kuna maradhi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ukimwi, lakini pia kuna suala la mimba zisizotarajiwa, hivyo nalazimika kujilinda na mambo yote hayo kikamilifu,” alisema Aslay.

Ally Katalambula

Leave A Reply