BBNaija Yarudi kwa Kishindo! Msimu wa 10 Wazinduliwa Rasmi Leo Nigeria
Tamasha maarufu la runinga barani Afrika, Big Brother Naija (BBNaija), limerudi kwa kishindo leo Julai 26, 2025, likianza msimu wake wa 10 kwa uzinduzi wa aina yake nchini Nigeria.
Kwa mara nyingine, watazamaji kutoka Tanzania hadi Nigeria wanashuhudia nyumba ya Big Brother ikifunguliwa rasmi, huku drama, mapenzi, usaliti na ushindani wa hali ya juu vikitarajiwa kuchukua nafasi kila siku kwa wiki 10 mfululizo.
Kilele cha msimu huu? Zawadi ya ₦150 milioni (sawa na zaidi ya TSh milioni 330)! Hii ndiyo zawadi kubwa zaidi kuwahi kutolewa kwenye historia ya BBNaija – ikijumuisha pesa taslimu na dili za ubalozi.
STORI NA ELVAN SITAMBULI | GPL
Comments are closed.