Benki Ya Exim Kuhudumia Sekta Kilimo cha Korosho

Benki ya Exim Tanzania mapema wiki hii ilishiriki kikamilifu kwenye mkutano mkuu wa wadau wa Korosho uliofanyika mkoani Lindi.
Pamoja na kuwa sehemu ya wadhamini wakubwa mkutano huo benki hiyo ilipata wasaa wa kuelezea fursa mbalimbali za kibiashara hususani katika zao hilo, mipango ya ukuaji na uboreshaji wa huduma inazotoa kwa wadau hao ikiwemo akaunti ya Mzalendo ambayo haina makato ya mwezi kwa wakulima hao.

Akizungumza kwenye mkutano huo uliohudhuliwa na wadau mbalimbali wa zao la korosho wakiwemo wakulima, viongozi wa kiserikali, wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya wakulima, Meneja wa Benki hiyo Tawi la Mtwara Bw Ramadhani Magera alisema benki hiyo imejipanga zaidi kutoa huduma zinazoendana na mahitaji ya wadau hao kwa wakati sahihi.

“Ukuaji wa benki ya Exim unaoshuhudiwa kwasasa ni matokeo ya ushirikiano baina yetu na wateja wetu wakiwemo wakulima ambao kwa kiasi kikubwa wameonyesha imani kubwa kwetu na hivyo kutuwezesha tuzidi kubuni huduma bora na rafiki za kibenki mahususi kwa ajili yenu ili kulinda na kurejesha imani mliyonayo kwetu,’’ alisema.

