HUU ni ushuhuda wa binti, SARAH CHARLES, mwenye umri wa miaka 18, ambaye hana mikono yote miwili, lakini pia hana miguu yote miwili.
Sarah alizaliwa akiwa na ulemavu huo mkoani Shinyanga. Pamoja na ulemavu huo, binti huyu haamini katika kushindwa. Anaweza kufanya baadhi ya mambo ya kushangaza. Na huu ni ushuhuda wa safari ya maisha yake ambao utakuwa funzo na hamasa kwa watu wengi.