The House of Favourite Newspapers
gunners X

Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari Yatangaza Ukaguzi Maalumu Nchini

0

Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari imetangaza kufanya ukaguzi maalumu katika vyombo vya habari na maeneo mbalimbali nchini, kwa lengo la kujiridhisha kuwa watu wote wanaotekeleza majukumu ya kihabari wanakidhi vigezo na matakwa ya kisheria.

Bodi hiyo imesema ukaguzi huo unalenga kuhakikisha taaluma ya uandishi wa habari inalindwa, maadili yanaimarishwa na sheria zinazingatiwa ipasavyo katika utekelezaji wa majukumu ya kihabari.

Kwa mujibu wa Bodi hiyo, imebaini kuwa baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu, baadhi ya watu wasiokuwa na sifa stahiki wameanza tena kujihusisha na kazi za kihabari, kinyume na taratibu na sheria zilizopo.

Hatua ya ukaguzi huo inalenga kudhibiti hali hiyo na kuhakikisha kuwa ni waandishi wa habari waliothibitishwa pekee wanaoruhusiwa kufanya kazi katika vyombo vya habari na maeneo mengine yanayohusiana na taaluma hiyo.

Bodi imewataka waandishi wa habari na vyombo vyao kushirikiana kikamilifu wakati wa zoezi hilo, huku ikisisitiza kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kukiuka sheria.

TRUMP AMDHIHAKI MADURO STAILI ya KUCHEZA – ADAI ALIWATESA RAIA KWENYE VITUO vya MATESO…. 📍USA

Leave A Reply