The House of Favourite Newspapers

MAKONDA: Unaiba Hati ya Mpenzi Wako? Tutawakomesha

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema serikali ya mkoa wake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi iliyopo chini ya Waziri William Lukuvi, imejiapanga vyema kukomesha vitendo vya utapeli vinavyofanyika kwa njia ya kuiba hati na kuipeleka benki kuchukulia mkopo vinavyofanywa na watu wa karibu na wenye nyumba hizo.

 

RC Makonda amesema kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo Ofisi yake imeandaa mkutano utakaohusisha Ofisi Yake, Wizara ya Ardhi na Taasisi za Kibenk kwa ajili ya kuzungumzia na kulipatia ufumbuzi suala hilo ambalo kwa kiasi kikubwa husababisha madhara makubwa kwa wananchi ikiwemo vifo vitokanavyo na mshtuko.

Comments are closed.