The House of Favourite Newspapers
gunners X

Brigedia Jenerali Mbungo Akabidhi Ofisi ya Takukuru

0

ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Julius Mbungo, jana Ijumaa Mei 21, 2021 amekabidhi rasmi ofisi kwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi Salum Rashid Hamduni.

 

Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za TAKUKURU zilizoko PCCB HOUSE Upanga Dar es Salaam na kushuhudiwa na na baadhi ya Wakurugenzi wa Taasisi hiyo.

 

Akizungumza na viongozi pamoja na watumishi baada ya makabidhiano hayo, Brigedia Jenerali Mbungo amesema anashukuru kwa ushirikiano alioupata kutoka kwa viongozi na watumishi wa TAKUKURU kwa kipindi cha miaka minne (2016–2021) alichokuwa katika taasisi hii na kwamba ushirikiano huo ndiyo uliomwezesha kuondoka TAKUKURU akiwa salama.

 

Leave A Reply