Bunge la Tanzania, UAE Kuanzisha Kamati Maalum ya Ushirikiano

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu akiwa na Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Mheshimiwa Lt. Jen. (Mst) Yacoub Hassan Mohamed walifanya mazungumzo na Spika wa Bunge la umoja wa Falme za Kiarabu, Saqr Bhogash katika ofisi za Bunge hilo Abu Dhabi Novemba 25, 2025.
Mazungumzo hayo yalijikita katika kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili hususan katika upande wa Mabunge.
Aidha, katika mazungumzo hayo imeazimiwa kuunda kamati ya kudumu ya ushirikiano baina ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu ambapo kamati hiyo pamoja na mambo mengine itaratibu masuala mbalimbali ya pamoja zikiwemo ziara za Wabunge na Viongozi wa Mabunge ya pande zote mbili za kubadilishana uzoeefu na mafunzo ya kujengeana uwezo katika masuala ya kibunge.


