Chama Apewa DK 270 Simba

KOCHA Msaidizi wa Simba, Seleman Matola, amefunguka kuwa bado kiungo wao mshambuliaji, Clatous Chama anahitaji michezo mingine mitatu ambayo ni sawa na dakika 270 ili kuwa timamu tofauti na sasa.
Chama tangu amerejea ndani ya timu hiyo kwenye usajili wa dirisha dogo uliofungwa Januari 15, mwaka huu, amefanikiwa kucheza michezo mitatu ya ligi kuu dhidi Mtibwa Sugar, Kagera Sugar na Prison, huku akiwa hajafunga bao wala kutoa asisti.

Kwenye Kombe la Shirikisho la Azam Sports dhidi ya Dar City, Chama alifanikiwa kufunga bao moja
na kutoa asisti mbili wakati Simba ikishinda 6-0.
Akizungumza na Spoti Xtra, Matola alisema: “Watu wanatakiwa kufahamu kuwa Chama anahitaji michezo
mingi zaidi ya mitatu ya kucheza ili kuwa bora zaidi.
“Mchezaji anahitaji kupata michezo mingi zaidi kuonesha ubora, hivyo hata kwa Chama ipo hivyo, anahitaji muda kidogo tu atakuwa bora zaidi.”
STORI: MARCO MZUMBE

