The House of Favourite Newspapers
gunners X

Chief Godlove na Mama Greyson Watembelea Kaburi la Mtoto Wao- Picha

0

 

Wazazi wa marehemu Greyson Kanyenye, Chief Godlove na Zainabu Shaabani ‘Jojo,’ walitembelea kaburi la mtoto wao.

Wazazi wa marehemu Greyson Kanyenye, Chief Godlove na Zainabu Shaabani ‘Jojo,’ walitembelea kaburi la mtoto wao walipokwenda kukamilisha ujenzi wa nyumba ya milele ya marehemu.

Baada ya ujenzi wa kaburi kukamilika, wazazi hao waliweka maua juu ya kaburi hilo, huku ikielezwa kuwa Chief Godlove ni baba mlezi wa mtoto huyo, ingawa hakuweza kuhudhuria mazishi kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake.

Mazishi ya Greyson yalifanyika kwa huzuni kubwa, yakihudhuriwa na wananchi waliokuwa wamegubikwa na simanzi, huku kifo chake kikileta mshtuko na taharuki kubwa katika jamii. Ibada ya kuuaga mwili wa marehemu ilifanyika nyumbani kwao, Mtaa wa Majengo Mapya, Area D, kabla ya safari ya kuelekea makaburini.

Mjomba wa marehemu, alipokuwa akisoma historia ya mtoto huyo, alielezea kwa majonzi jinsi Greyson alivyouawa kikatili, huku akisisitiza umuhimu wa haki kutendeka kwa waliohusika.

Greyson, aliyekuwa na umri wa miaka sita, aliuawa kwa kuchinjwa na kupigwa na kitu kizito kichwani mnamo tarehe 25 Desemba 2024, na alizikwa jioni ya tarehe 26 Desemba 2024 katika makaburi ya Bambalaga, jijini Dodoma.

Kiongozi wa dini kutoka kanisa alilokuwa akihudhuria marehemu alimuelezea Greyson kama mtoto mwenye heshima, mcha Mungu, na aliyekuwa na bidii katika kuimba kwaya ya kanisa.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi, uchunguzi kuhusiana na tukio hili la kusikitisha bado unaendelea.

CHIEF GODLOVE – ”NATAMANI NIKUTANE na MUUAJI ANIELEZEE – MAMA GREYSON HAKULA TANGU JUZI”…


 

Leave A Reply