The House of Favourite Newspapers
gunners X

Chipolopolo Yampa Mzuka Chirwa

0

BAADA ya kuitwa kwa mara ya kwanza kwenye timu ya Taifa ya Zambia ‘Chipolopolo’, straika wa Azam FC, Obrey Chirwa amefunguka kuwa ataendelea kujituma ili aendelee kuitwa kwenye timu hiyo kwa mara nyingine.

 

Staa huyo wa Azam ameitwa kwenye kikosi cha Chipolopolo kwa ajili ya mechi za timu hiyo ambazo watacheza dhidi ya Congo Oktoba 7, Kenya Oktoba 11 na Afrika Kusini Oktoba 13.

 

Chirwa ameliambia Championi Jumamosikuwa, kwake ni jambo zuri ambapo ataendeleza moto wake katika Ligi Kuu Bara kwa ajili ya kupata nafasi ya kuitwa tena kwa mara nyingine.

 

“Najisikia vizuri, muda mrefu sijacheza timu ya taifa nilicheza chini ya miaka 20 na 23, najisikia furaha sana.

 

Hii ni mara ya kwanza kuitwa timu hiyo ya wakubwa.“Kuhusu mechi hizo, siyo ndogo kwa sababu hadi unaitwa timu ya taifa ni kuonyesha umeaminiwa na lazima uonyeshe kwenye timu ya taifa kwa sababu hata klabu yangu itakuwa inaniangalia.

 

“Nitaendelea kufunga na kuasisti mara kwa mara kwa ajili ya kunifanya niitwe katika timu ya taifa kila mara,” alimaliza Chirwa.

STORI: SAID ALLY, Dar es Salaam

Leave A Reply