The House of Favourite Newspapers

CHUO CHA KILIMANJARO CHAENDELEA KUPOKEA WANAFUNZI

Muonekano wa KITM.

Chuo cha Kilimanjaro Institute of Technology and Management (KITM) kilichopo katika jengo la Mama Ngoma, Mwenge na Afrikasana, Sinza jijini Dar es Salaam, kimeendelea kutoa nafasi kwa wahitimu wahitimu wa kidato cha nne, sita na wengine ambao wangependa kujiendeleza kitaaluma katika ngazi ya cheti (certificate) na stashahada (diploma) katika kozi mbalimbali zikiwemo za mapishi,  uongozi, biashara, ufundi umeme, magari, kompyuta, udereva na nyinginezo.

Wanafunzi wa mapishi wakitabasamu baada ya kumaliza kupika kwa ufasaha chipsi na kuku.

Nafasi hii ni kwa wahitimu wote wanaotaka kuendelea na masomo, hata kama ufaulu wao haukuwa wa kuridhisha, kufika chuoni hapo na kujadiliana na walimu wazoefu kuona jinsi ya kuwasaidia wanafunzi hao wenye nia ya dhati na masomo ili kutimiza ndoto zao.

 

Katika chuo cha KITM zipo kozi za muda mfupi kuanzia miezi mitatu mpaka kozi za muda mrefu zinazochukua miaka miwili ambazo Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), Biashara, Uhasibu na Ufundi Umeme, kimeendelea kujipatia sifa za kipekee kutokana na wahitimu kutoka chuoni hapo, kuendelea kupata nafasi nyingi na kufanya vyema katika soko la ajira serikalini kwenye makampuni na mshirika binafsi.

Wanafunzi wakijisomea kwenye maabara ya computer.

 

Kozi zingine ni Usimamizi wa Biashara (Business Management), Uhazili (Front Office and Secretarial) na Usimamizi wa Hoteli na Kuongoza Watalii (Hotel Management and Tour Guide), Accountacy na Procurement and Supply, Umeme, Kozi za Kompyuta, Graphics Designing, Website Designing, Programming, Database, PC Maintanance, CISCO Certification, Microsoft Certification na nyingine nyingi.

 

Mwalimu akimuelekeza mwanafunzi wa kozi ya ufundi umeme namna bora ya kuunganisha mfumo wa umeme jengo.

 

KITM kimesajiliwa na VETA na NACTE na kupewa namba ya usajili, REG/ANE/029, kinatoa mafunzo yake kwa vitendo ambapo walimu waliobobea, wanawafundisha wanafunzi kwa vitendo na kuwapa uwezo wa kuelewa kwa urahisi kile wanachofundishwa darasani.

 

Kwa wanafunzi wa masomo ya teknolojia, chuo hicho kina maabara na vifaa vya kutosha ambapo kila mwanafunzi hupata nafasi ya kufanya kwa vitendo masomo yanayotolewa, ikiwa ni pamoja na kuunganisha mifumo ya intaneti na kamera za usalama (CCTV), huku pia kukiwa na maktaba iliyosheheni vitabu mbalimbali ambavyo ni nyenzo kubwa ya kuwaongezea maarifa na ujuzi katika taaluma zao.

Mwanafunzi wa kozi ya ufundi umeme akijifua kwa vitendo.

Kwa upande wa wanafunzi wanaosomea masomo ya hoteli na kuongoza watalii, chuo hicho kina utaratibu maalum wa kuwapeleka wanafunzi wake kufanya mazoezi kwa vitendo kwenye mahoteli makubwa, hivyo kuwaongezea ‘exposure’ na uelewa wa kile wanachofundishwa darasani.

 

Tofauti na vyuo vingine ambavyo ni lazima mwanafunzi alipe ada yote ndipo aendelee na masomo, KITM hutoa fursa ya wanafunzi na wazazi kulipa ada kidogokidogo kwa awamu, hivyo kuondoa usumbufu wa mwanafunzi kukosa masomo kwa sababu ya kutokamilisha ada yake.

Wanafunzi wa kozi ya kompyuta wakiwa darasani wakisoma kwa vitendo.

Vyeti vinavyotolewa kwa wahitimu wa cheti hicho, vinatambulika na vyuo vingine vikubwa nchini pamoja na vile vya nje ya nchi, hivyo kuwapa urahisi wanafunzi wanaopenda kuendelea na masomo ya juu zaidi, ndani ya nje ya nchi na pia kupata ajira kwa urahisi kwa wale wanaotaka kuingia kwenye ajira.

 

Kwa kuzingatia uhitaji wa waajiriwa wanaohitaji kujiendelea kimasomo, chuo hicho pia kinatoa mafunzo maalum ya jioni (evening programs) ambapo kwa wale wanaofanya kazi, wanaweza kuingia darasani baada ya muda wa kazi na kufundishwa na walimu wazoefu hivyo kuokoa muda.

Wanafunzi wa kozi ya mapishi, KITM kampasi ya Sinza-Mapambano jijini Dar wakiwa kwenye mafunzo ya kupika kwa vitendo.

Pia chuo hicho kimezindua kozi nyingine mpya ambazo ni pamoja na Electrical Installation (Ufundi Umeme) na Video Production, wakitumia motto wao wa ‘KITM Elimu Na Ujuzi Kwa Maendeleo Ya Viwanda’.

 

Kama unahitaji mahali pa kuongezea ujuzi wako, basi Kilimanjaro Institute of Technology ndiyo chaguo lako.

Kwa mawasiliano;

Simu: +255 717 816034 / +255 766 348652
Email: [email protected]

KWA MAELEZO ZAIDI TEMBELEA ==> Kilimanjaro Institute of Technology and Management (KITM)

Comments are closed.