DC Magoti Alivyowapa Onyo Kali Watakaosababisha Uzembe Kwenye Elimu ya Watoto Wao

Kisarawe, Pwani. 12 Februari 2025: Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Petro Magoti amewaonya wazazi watakaofanyia mzaha elimu za watoto wao ikiwemo kutohakikisha watoto hao wanafika shuleni na kusababisha watoto wadogo na wanafunzi kupata mimba na kukatiza masomo.

DC Magoti amesema pamoja na kuhakikisha watoto hao wanafika shuleni kwa wakati amesisitiza kuwa na wale waliochaguliwa kukaa hostel nao pia wakae hostel na sio kukaa majumbani maana kuna wengine wanaotokea majumbani wanaishi kwa wanaume.

DC Magoti alisema hayo wakati akipokea msaada wa bati 400 zenye thamani ya zaidi ya pesa za kitanzania milioni 16 zilizotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya shule za wilaya ya Kisarawe.
Baada ya kupokea msaada huo DC Magoti alimshukuru Meneja wa benki hiyo Kanda ya Dar es Salaam Seka Urio aliyeiwakilisha benki hiyo kukabidhi msaada huo.

Meneja Urio kwa upande wake amesema msaada huo ni miongoni mwa fadhila zake kwa jamii wanayoihudumia na anaamini kwa kuezeka mapaa mazuri kwenye madarasa yaliyokuwa yakivuja wakati wa mvua na kuwafanya wanafunzi washindwe kusoma vizuri sasa sehemu tatizo hilo litakuwa limemalizwa.
Pamoja na madarasa bati hizo zitakwenda kuezeka nyumba za walimu ambazo nazo zinachangamoto ya mapaa. HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA NEEMA ADRIAN


Comments are closed.