Dkt. Biteko: Tuvumiliane Na Kuheshimiana Kama Watanzania – Video

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewaasa Watanzania kuishi kwa kuvumiliana, kuheshimiana na kupendana kama ilivyoagizwa na vitabu vya Mungu.
Dkt. Biteko amesema hayo Septemba 15, 2024 katika Kongamano la Tano la Ekaristi Takatifu Kitaifa lililofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaaam.

“ Wote tuliokuja hapa tumesikia mahubiri mazuri, tumehubiriwa kuwa wamoja zaidi tukavimiliane zaidi na kuheshimiana kama Watanzania wamoja. Kuwa na mawazo tofauti kusitufanye tugawanyike Ekaristi Takatifu hii itufanye tuwe wamoja,” amesema Dkt. Biteko.
Amesisitiza “ Tuwafundishe jamii tuliyonayo kuwa na huruma kwa watu wote wanaohitaji na muhimu zaidi kuwa na huruma na taifa letu la Tanzania.”


