The House of Favourite Newspapers
gunners X

Dkt. Mwigulu Ashiriki Mazishi Ya Jenista Mhagama, Atoa Maagizo Kwa Mkandarasi Wa Barabara Ya Kitai–Ruanda (Picha +Video)

0


Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba leo Desemba 16, 2025 ameshiriki katika Mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Marehemu Jenista Mhagama, yaliyofanyika katika Kijiji cha Ruanda Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma

Akizungumza katika mazishi hayo, Dkt. Mwigulu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed kumsimamia mkandarasi anayejenga barabara ya Kitai hadi Ruanda ili akamilishe ujenzi wa barabara hiyo muhimu kwa wakazi wa mkoa huo.

Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema tayari Serikali ilikwisha kutoa fedha za ujenzi wa barabara hiyo kwa kutambua umuhimu wake kwenye uchumi wa mkoa huo na Taifa kwa ujumla.

“Ni dhahiri kabisa kwamba kasi ya ujenzi hairidhishi nikutake mkuu wa mkoa, mwite mkandarasi huyu mara baada ya shughuli hii, mwambie alishapokea fedha sasa afanye kazi ionekane, kama ameshatumia pesa hiyo kwenye kazi nyingine kamata passport yake asitoke mpaka kazi hii ikamilike”

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi aliwaongoza waombolezaji kwenye mazishi hayo.

Leave A Reply