The House of Favourite Newspapers

Dstv Yazindua Msimu Wa Tatu ‘Kipindi Cha Harusi Yetu’

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza.

KAMPUNI ya Multichoice Tanzania jana imezindua msimu mpya wa Kipindi cha Harusi Yetu ambacho hurushwa katika king’amuzi chake kwenye chaneli namba 160.  Uzinduzi huo umefanyika katika hoteli ya Coral, Masaki jijini Dar.

Mkuu wa chaneli ya Maisha Magic Bongo, Barbara Kambogi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa chaneli ya Maisha Magic Bongo, Barbara Kambogi, alisema baada ya kipindi hicho kuonekana kuwa na mashabiki wengi ambao walikuwa wakikifuatilia kwa ukaribu zaidi, wamelazimika kuzindua sehemu hiyo ya tatu ili waweze kuwaonyesha maudhui bora zaidi.

Mtangazaji wa msimu mpya wa Kipindi cha Harusi yetu, Victoria Simon (katikati).

Pamoja na uzinduzi huo pia Kambogi ameeleza kuwa kwa muda wote sasa watakuwa wakiendelea kushirikiana kwa karibu zaidi na waigizaji wote nchini ili waweze kuitumia chaneli hiyo kutangaza kazi zao.

Baadhi ya wasanii waliocheza tamthilia ya Uber na Mwantumu.

Dstv  wana vipindi kibao ambavyo hurusha tamthilia na filamu mbalimbali za nchini ikiwemo ya Uber na Mwantumu ambazo zinafanya vyema.

PICHA: MUSA MATEJA | GPL

Comments are closed.