The House of Favourite Newspapers

Efm, DTB kutekeleza agizo la Rais Magufuli Desemba 9

1

efm (1)

Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Efm Radio, Denis Ssebo akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

Efm radio kwa kushirikiana na Benki ya DTB pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni chini ya mkuu wa wilaya hiyo, Paul Makonda wameamua kuunga mkono na kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli la kuadhimisha siku ya Uhuru Desemba 9, mwaka huu kwa kufanya usafi wa mazingira.

Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kuondoa ama kumaliza kabisa tatizo la magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.

Akizungumza leo katika ofisi za Efm zilizopo Kawe jijini Dar, Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa Radio hiyo, Denis Ssebo amesema siku hiyo wameipa kauli mbiu ya “Naona aibu kuishi na uchafu” wakiunga mkono kauli mbiu ya Wilaya ya Kinondoni inayosema “Usafi uanze na mimi”.

Maeneo wanayotarajia kuyafanyia usafi ni barabara inayoanzia Morocco kuelekea Magomeni, kuanzia saa 2 asubuhi na kuendelea, hivyo amewaomba kutumia nafasi hiyo kuwaomba wateja wa Benki ya DTB na wasikilizaji wa Efm pamoja na wakazi wa Wilaya ya Kinondoni kujitokeza siku hiyo ya Uhuru kwa usafi wa mazingira ya nchi.

1 Comment
  1. Kabagala says

    I think ndiyo tumepata uhuru xaxa!

Leave A Reply