GUERRA de El Clasico yaani Vita ya El Clasico ndiyo habari ya leo. Guerra de El Clasico ni maneno ya Lugha ya Kihispaniola inayomaanisha vita ya mechi ya wababe wa soka nchini Hispania ambao ni Real Madrid na Barcelona.
Dunia kidogo itasimamisha mambo yake na mashabiki wengi wa soka watatazama mechi ya Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’ kati ya Barcelona na Real Madrid kwenye Uwanja wa No Camp leo saa 12:30 jioni. Hii ni moja kati ya mechi kali za watani wa jadi duniani na inaweza kuwa ya kwanza katika miaka ya hivi karibuni, kwani nyingine sasa zinaonekana ni za kawaida na zilizokosa mvuto.
Mechi ya kwanza ya El Clasico ilichezwa mwaka 1902. Huo ulikuwa mchezo michuano ya Kombe la Ligi ambapo Barcelona ilishinda mabao 3-1, hata hivyo mechi ya kwanza ya La Liga kati ya timu hizo ilichezwa Agosti 17, 1929 ambapo Madrid ilishinda mabao 2-1.
Hadi sasa mechi 264 za El Clasico zimechezwa ambapo Barcelona imeshinda 109, Madrid 97 na zilizobaki 58 ni sare. Ila katika La Liga, Madrid ndiyo vinara kwani katika mechi 172, wao wameshinda 72, Barcelona imeshinda 68 na 32 ni sare. Hii ni zaidi ya mechi katika La Liga pia kati ya mechi zinazofuatiliwa zaidi Ulaya na duniani kote kila zinapochezwa.
KATIKA LA LIGA
Hadi sasa Madrid ndiyo kinara katika La Liga kwani ipo kileleni ikiwa na pointi 33 ikiwa haijafungwa hata mechi moja katika michezo 13 iliyocheza ambapo imeshinda kumi na kutoka sare mitatu tatu.
Barcelona yenyewe ni ya pili ikiwa na pointi 27, lakini imeshinda mechi nane kati ya 13 ilizocheza huku ikitoka sare tatu na kupoteza mara mbili.
Madrid ina mabao 36 ya kufunga wakati Barcelona wanayo 33 tu, hii inaonyesha kwa kiasi fulani fowadi ya Madrid inayoongozwa na Cristiano Ronaldo ipo vizuri kulinganisha na ile ya Barcelona iliyo chini ya Lionel Messi.
Pia hata safu ya ulinzi ya Madrid nayo imeruhusu mabao 11 tu wakati ile ya
Barcelona ikiwa imeruhusu mabao 14, hivyo ukuta wa Madrid chini ya Sergio Ramos upo vizuri kuliko ule wa Barcelona chini ya Gerald Pique.
HATARI YA RONALDO
Kati ya mabao 36 ya Madrid, 10 amefunga Ronaldo hiyo ni sawa na asilimia 30.3, hapa utaona ni kwa jinsi gani Ronaldo alivyo mtu muhimu katika kikosi chao.
Kwenye kikosi cha Barcelona, kati ya mabao 33, tisa amefunga Messi na nane
amefunga Luis Suarez, hapa unapata picha kwamba Barcelona ina wigo mpana wa
kupata mabao kuliko Madrid.
Ukimtoa Ronaldo, mchezaji anayefuatia kwa kufunga Madrid ni Gareth Bale mwenye mabao matano halafu Alvaro Morata yeye ana mabao manne.
Hii ina maanisha kwamba, Ronaldo anaweza kuwa mwiba mchungu kwa Barcelona
lakini likitokea tatizo na akakosekana katika mchezo huu, inaweza kuwa tatizo kubwa kwa Madrid.
VITA YA CASEMIRO, RAKITIC
Wengi wanadhani mechi hii hubeba upinzani kati ya Ronaldo na Messi, lakini kuna kitu huwa kinasahaulika
hicho ni kivumbi cha viungo wakabaji ambapo kwa Madrid yupo Casemiro na Barcelona wanao Ivan Rakitic na Sergio Busquets.
Kocha wa Madrid, Zinedine Zidane alipanga kumtumia Casemiro ambaye jina halisi ni Carlos Henrique
Jose Francisco Venancio Casimiro katika mchezo wa Jumatano wiki hii wa Copa del Rey dhidi ya Cultural
Leonesa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Casemiro alikuwa majeruhi na sasa amerejea uwanjani na atakutana na Rakitic katika mechi ya leo, wawili hawa wanasifi ka kwa ukabaji yaani ni mafundi wa ‘kukata umeme ’ ,
h i v y o
tutarajie burudani kali. Pia beki Raphael Varane naye emerejea katika kikosi cha Madrid akitokea katika ma jeruhi.
ZIDANE, LUIS ENRIQUE WABABE WA AL CLASICO
Hii ni mechi nzuri kwa makocha Zidane wa Madrid na Luis Enrique wa Barcelona kwani wote wana kitu wanachokijua katika El Clasico kwa kucheza wenyewe pia wakiwa makocha.
E n r i q u e ana faid a m o j a kubwa kwamba aliichezea Madrid kati ya mwaka 1991 hadi 1996 akicheza mechi 157 na kufunga mabao 15 akiwa kama kiungo mshambuliaji kisha akajiunga na Barcelona kati ya mwaka 1996 hadi 2004, hapo alicheza mechi 207 na kufunga mabao 73.
Tofauti na Zidane, Enrique amepitia falsafa za timu zote mbili hivyo ana kitu zaidi anachokifahamu kwa timu hizo. Zidane alicheza Madrid kati ya mwaka 2001 hadi 2006 ambapo alicheza mechi 155 na kufunga mabao 37.
“Tunakwenda kwenye mechi kubwa, hapa unatakiwa utilize kichwa sana kwa maana wengi wanaitazama mechi hii nayoweza kuamua bingwa wa ligi, hivyo tutakuwa makini,” anasema Zidane.
Kwa upande wake, Enrique anaamini kwamba haitakuwa vyema kwake kupoteza mechi tatu ikiwemo moja dhidi ya Madrid; “Tumepoteza mechi mbili tayari, kufungwa na Madrid itakuwa tatizo zaidi kwetu, hapo unaona ugumu wa mechi hii.”
Wakati Madrid ikicheza na Cultural Leonesa katika Copa del Rey, Barcelona yenyewe katikati ya wiki hii ilicheza na Hercules katika michuano hiyo na Enrique aliwaweka benchi nyota wake kadhaa.
MESSI MKALI WA RONALDO
Katika mechi za El Clasico, Messi anaon goza
kwa ufungaji akiwa kila alipokutana nayo. Madrid, huyu alifunga mabao 18 ambapo kati yake 14 ni ya katika La Liga.
Ronaldo yeye amefunga mabao 16 katika El Clasico Messi katika El Clasico.
MWAMUZI UTATA
Mwamuzi Carlos Gomez ndiye aliyetajwa kuchezesha mechi hii Clasico kuna utata kwamba amekuwa Akiipendelea Barcelona Japokuwa hakuna kauli ya malalamiko ya moja kwa moja lakini inaonekana Gomez ana kismati zaidi na Barcelona hivyo kutoa mwanga wa Madrid kuwa katika wakati mgumu leo.




Comments are closed.