The House of Favourite Newspapers

Father Atembea na Kiti cha Urais Azam FC, Popat na Kuwe Wapewa Umakamu

0

BODI ya klabu ya Azam Fc imefanya mabadiliko ya kimuundo na mfumo wa klabu hiyo yanayohusu nafasi za juu za utendaji katika utawala ambapo nafasi ya Mwenyekiti wa klabu imebadilika mara moja na kuwa Rais wa klabu (Club President).

Taarifa ya leo Septemba 9, 2025 iliyotolewa na Menejimenti ya Azam Fc imeeleza kuwa Rais wa klabu hiyo anabaki kuwa Nassor Idrissa maarufu kama Father ambaye atakuwa na makamu wawili.

Nafasi ya Makamu wa Rais anayeshughulika na timu kubwa (Vice President – Senior Team) itashikwa na Abdulkarim Nurdin maarufu kama Popat huku nafasi ya Makamu wa Rais anayeshughulika na akademi (Vice President – Academy) ikishikwa na Omary Kuwe.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kutokana na mabadiliko hayo, nafasi ya Mtendaji Mkuu (CEO) itajazwa baadaye lakini kwa sasa, Abdulkarim Nurdin, ataikaimu hadi atakapopatikana mtendaji mwingine.

Aidha, Mkurugenzi wa Fedha, Abdulkarim Shermohamed maarufu kama Karim Mapesa, ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi.

Leave A Reply