The House of Favourite Newspapers

FIFA Yazindua Mpira Mpya “Trionda” kwa Kombe la Dunia 2026

0

Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, limezindua rasmi mpira wa mashindano ya Kombe la Dunia 2026 unaojulikana kama “Trionda”, mpira wenye teknolojia ya kisasa itakayosaidia wachezaji, washabiki na VAR (Video Assistant Referee).

Jina Trionda, kutoka Kihispania, linamaanisha “mawimbi matatu,” ikionyesha kuwa mashindano hayo yataandaliwa na nchi tatu: Canada, Mexico, na Marekani. Mpira huo una rangi tatu – nyekundu, kijani, na bluu – zikionyesha kila nchi inayoshirikiana katika maandalizi ya Kombe la Dunia.

Aidha, mpira una nembo maalumu zinazowakilisha nchi tatu:

Nyota – Marekani

Lotus – Canada

Mamba – Mexico

Trionda pia ina teknolojia ya hali ya juu itakayorahisisha utambuzi wa faulo na kugundua mguso wa mkono au kosa la mchezaji, huku taarifa zikitumwa moja kwa moja kwa VAR kwa haraka.

Rais wa FIFA, Gianni Infantino, alisema:

“Trionda inafurahisha sana. Ni ishara ya umoja na mshikamano kati ya nchi tatu za mwenyeji wa Kombe la Dunia 2026.”

Mpira huu unatarajiwa kuleta mapinduzi katika mchezo na kuongeza uwazi, haki, na burudani kwa mashabiki wa soka duniani kote.

Leave A Reply