Jeshi la Pakistan Limetoa Amri ya Kufanyika Uchunguzi wa Mauaji ya Mwandishi Nchini Kenya

JESHI la Pakistan limetoa amri ya kufanyika uchunguzi wa mauaji ya mwandishi wa habari, Arshad Sharif ambaye ni raia wa Pakistan aliyeuawa na Polisi nchini Kenya.

Taarifa hiyo imetolewa leo na kudai kuwa mwandishi huyo alijificha Kenya baada ya kukimbia nchini kwao Agosti, mwaka huu kwa sababu ya kulikosoa Jeshi la Pakistan.
Hayo yamejiri baada ya madai ya uchochezi ya kuwashutumu majenerali wa jeshi kwa kumuondoa Waziri Mkuu wa zamani, Imran Khan.

Msemaji wa Jeshi la Pakistan, Jenerali Babar Iftikhar amesema kuna umuhimu kwa taasisi za kimataifa kama Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi wa uwazi.
Kwa mara ya kwanza kwenye historia ya taifa hilo Mkuu wa Idara ya ujasusi (ISI) amezungumza na waandishi wa habari na kusema hakukua na kitisho chochote dhidi ya maisha ya Sharif na alikuwa akiwasiliana na marafiki zake waliopo kwenye idara hiyo.
Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao

