Jino la Waziri Mkuu wa Kwanza wa Congo Kurudishwa Kutoka Ulaya

UBELGIJI itamrudishia rasmi Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi jino ambalo Kamishna wa Polisi wa Ubelgiji anadai ililitoa kwenye mwili wa Patrick Lumumba alipomsaidia kutoweka.
Lumumba alikuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka 1960 kabla ya kuuawa baada ya kuongoza harakati za kugombea uhuru kutoka kwa utawala wa kikoloni (Ubelgiji).
Baada ya kuahirishwa mara kadhaa kwa sababu za kama vile janga la UVIKO-19 na mipango ya makumbusho, urejeshwaji wa jino hilo sasa umepangwa Juni 20, 2022.

Watoto wa Lumumba watakuwa sehemu ya ujumbe wa Congo ambao utapokea mabaki hayo, kama sehemu ya hafla binafsi ya kifamilia kama walivyotaka; Waziri Mkuu wa Ubelgiji alisema katika taarifa yake.
Naye Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Congo, Catherine Katsungu Furaha amesema nchi hiyo ina wajibu wa kurejesha mabaki ya mwili na kuzika katika ardhi ya Congo ili kuruhusu familia yake ya damu kumaliza maombolezo yaliyodumu kwa miongo kadhaa kwa kuwa hawakuuona mwili wa mpendwa wao huyo.
“Ni katika hali hiyo ambapo Serikali ya Congo imeungana na familia hiyo ili kujibu ombi lao la kuwapa heshima inayostahili. Kama shujaa wa Taifa anahitaji kutambuliwa hivyo,” anasema waziri huyo.