The House of Favourite Newspapers
gunners X

Jinsi ya kupika makaroni ya nyama ya kusaga

0

Ni Jumamosi nyingine tena mpenzi msomaji tunakutana kwenye safu hii ya Mapishi ya Leo ambapo tunaangalia jinsi ya kupika makaroni ya nyama ya kusaga, pishi hili tunalirudia kutokana na wasomaji wengi kuomba lirudiwe ili twende pamoja.

MAHITAJI
Pakiti moja ya makaroni
Pilipili manga iliyosagwa.
Chumvi
Blue band
Nyama ya kusaga
Kitunguu maji kimoja (kikate vipande vidogovidogo)
Vitunguu swaumu (vilivyosagwa)
Tangawizi (iliyopondwa)
Viazi (vikate vipande vidogovidogo)
Biringanya (ikate vipande vidogovidogo)
Pilipili hoho (ikate vipande vidogovidogo)
Pilipili kali (iache nzima)
Karoti (ikate vipande vidogovidogo)
Nyanya  (zikate vipande vidogovidogo)
Tui la nazi

JINSI YA KUPIKA MAKARONI
Andaa sufuria safi, weka maji ya kutosha.
Weka chumvi kiasi na pilipili manga iliyosagwa kisha bandika jikoni na yaache mpaka yachemke.
Maji yakishachemka weka makaroni ndani yake, yaache yaive.

Baada ya kuiva ipua, mimina makaroni kwenye chujio ili kuchuja maji uliyochemshia.
Chukua maji ya uvuguvugu miminia juu ya makaroni yakiwa bado kwenye chujio.

Rudisha sufuria uliyochemshia makaroni jikoni huku ukiwa umeweka moto mdogo sana.
Weka blue band kwenye sufuria yako jikoni na iacha iyeyuke vyema, kisha mimina makaroni ambayo tayari yameshajichuja maji.

Koroga vyema kwa dakika tatu ili mchanganyiko wa makaroni na blue band ukolee vyema.
Na hapo makaroni yako yatakuwa tayari.

Wiki ijayo tutaangalia jinsi ya kupika rosti ya nyama ya kusaga.

SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply