JKU vs Yanga Kukiwasha leo Fainali ya Muungano Cup 2025 Gombani

JKU SC vs Yanga SC zinatarajiwa kushuka Uwanja wa Gombani leo Mei Mosi kwenye mchezo wa fainali Muungano Cup 2025.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa 1:15 kwa wababe hawa wawili kushuka uwanjani katika kusaka mshindi atakayetwaa taji hilo.
JKU SC iliwaondoa Azam FC kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo huo Azam FC walianza kupata bao la uongozi na JKU SC wakasawazisha na kupata bao la ushindi.
Ilikuwa ni Aprili 28 2025, Azam FC waliumaliza mwendo kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Gombani ukisoma JKU SC 2- 1 Azam FC ni dakika ya 15 Yeison Fuentes wa Azam FC alipachika bao la uongozi ambalo lilidumu mpaka dakika ya 50.

Neve Adelin wa JKU SC alipachika bao la usawa na bao la ushindi likafungwa na Fredy Seleman dakika ya 80 likiwafungashia virago matajiri wa Dar.
Yanga SC iliwaondoa Zimamoto kwa ushindi wa penati 3-1 baada ya kutoshana nguvu kwa kufugana bao 1-1 hatua ya nusu fainali mchezo uliochezwa Aprili 29 2025.
Kwenye mchezo wa nusu fainali iliyochezwa Uwanja wa Gombani, ni Maxi Nzengeli alianza kupachika bao la uongozi kwa Yanga dakika ya 29 likawekwa usawa na Said Mwinyi wa Zimamoto dakika ya 71.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.


Comments are closed.