Kagere: Nataka Kuvunja Rekodi Ya Mabao
MEDDIE Kagere, mshambuliaji wa Simba amesema kuwa anashukuru kwa kuifungia mabao timu yake na anafikiria kuendelea kufanya hivyo pale atakapopata nafasi ili kuvunja rekodi yake ya msimu uliopita.
Katika ushindi wa mabao 8-0 mbele ya Singida United, juzi kwenye Uwanja wa Uhuru, Kagere alifunga mabao manne na kufikisha mabao 19 akiwa kinara wa utupiaji wa mabao ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu, akiwa amebakiza mabao manne kufikisha mabao 23 aliyofunga msimu wa 2018/19.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Kagere alisema kuwa anafurahi kuifungia mabao timu yake na kuipa ushindi kutokana na kazi yake.
“Ninafurahi kufunga na ninapenda kufanya hivyo kwa ajili ya timu yangu, nikipata nafasi ya kufunga nitafanya hivyo napenda kuona ninafunga zaidi hata ya msimu uliopita,” alisema.
Simba ikiwa imefunga mabao 63, Kagere amehusika kwenye mabao 24 akifunga mabao 19 na kutoa pasi tano za mabao.
MAPOVU YA MASHABIKI WA YANGA BAADA YA KUFUNGWA NA KMC (1-0)



