Kamanda SACP Richard Apinga Maandamano Atoa Wito Wa Kulinda Amani Wakati Wa Uchaguzi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Richard Abwao ametoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Tabora na Tanzania kwa ujumla kupuuza wito wa maandamano unaosambazwa kupitia mitandao ya kijamii.
Kamanda Abwao amesema maandamano hayo hayana msingi wa kisheria yanakiuka utaratibu uliowekwa, na yanaweza kupelekea kuvuruga amani ya nchi hasa wakati huu ambapo taifa linaelekea kwenye uchaguzi mkuu.
Kauli hiyo imetolewa wakati wa mazoezi ya utayari yaliyofanyika Oktoba 24, 2025 katika Manispaa ya Tabora, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kulinda amani kuelekea uchaguzi mkuu 29 octoba

Kamanda Abwao ameongeza kwa kusema tunaendelea kuimarisha usalama wananchi wakae wakifahamu kuwa uchaguzi ni haki ya kila mmoja, lakini tunapaswa kuuheshimu na kuufanikisha kwa amani, sio kwa maandamano.
Aidha, amewataka Maofisa na Askari wa Jeshi la Polisi mkoani humo kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uaminifu, na utii kwa sheria kuhakikisha kila mwananchi anashiriki uchaguzi katika mazingira ya utulivu.


