The House of Favourite Newspapers

Kapuya Aibukia Uwanjani KMC vs Simba

0

WAZIRI wa zamani wa Michezo na shabiki wa timu ya Simba, Profesa Juma Kapuya ametinga katika uwanja Ali Hassan Mwinyi Tabora na kutoa utabiri wake Kapuya ametabiri timu ya Simba kushinda bao 2-0 dhidi ya KMC katika mchezo wa ligi Kuu ya NBC.

Amesema kama ikitokea KMC wakapata bao moja, basi Simba itashinda kwa bao 3-1. “Kwa ufupi Simba itapata ushindi wa tofauti ya bao mbili dhidi ya wapinzani wetu,” amesema.

Profesa Kapuya amesafiri kutoka wilayani Kaliua kuja kuangalia mchezo huo akiwa anajulikana kama shabiki kindakindaki wa mabingwa hao wa soka nchini.

Hata hivyo mechi hiyo imeisha kwa Simba kuifunga KMC bao 4-1, mabao ambayo yamefungwa na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Joash Onyango na Kibu Denis ambaye amefunga mabao mawili.

Leave A Reply