The House of Favourite Newspapers

Karikoo: Waziri Mkuu kuongoza kutoa heshima za mwisho kwa waliofariki Mnazi Mmoja, Dar

0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema kuwa miili 13 ya waliothibishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kufariki baada ya ghorofa kuporomoka Kariakoo itaagwa katika Uwanja wa Mnazi Mmoja kuanzia saa 7 mchana mpaka saa 10 jioni.

Akizungumza na wanahabari usiku wa kuamkia Jumatatu Novemba 18, 2024 , RC Chalamila amesema kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ndiye atakayeongoza zoezi la kuaga miili hiyo, huku akiwaalika watu wote walioguswa na msiba huo kuhudhuria kutoa heshima za mwisho kwa marehemu wote.

“Inawezekana ratiba hii imekuwa ya haraka lakini ni kwasababu ya maombi ambayo yamefanywa na baadhi ya ndugu wa marehemu na kutokana pia na ushauri wa kitabibu uliotolewa na madaktari kuhusiana na namna tunavyoweza kuikabidhi miili hii kwa wenzetu wapendwa ambao wanatamani sasa kuwasindikiza marehemu”, ameeleza Chalamila.

Aidha amesema kuwa ndugu wote wa marehemu wanatakiwa kufika Hospitali ya Amana saa mbili kamili asubuhi ambapo watakutana na Mganga Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kupewa utaratibu wote wa kukabidhiwa miili ya ndugu zao.

Hata hivyo RC Chalamila amewatoa hofu wananchi kuwa zoezi la kuaga marehemu halitasitisha uokoaji ambao bado unaendelea katika jengo hilo lililoporomoka kama ikibainika bado kuna watu waliokwama ndani.

RAIS SAMIA KUHUSU KARIAKOO – ”13 WAFARIKI DUNIA – 80 WAMEOKOLEWA – TUTABEBA GHALAMA”

Leave A Reply