The House of Favourite Newspapers
gunners X

Kocha wa Liverpool Aionya Arsenal EPL… Atamba Kuibuka na Ushindi Jumapili Hii

0
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp.

JURGEN Klopp, amesisitiza kuwa, wana nafasi kubwa ya kuwapiga vinara wa Premier League, Arsenal, wikiendi hii.

Jumapili ya wikiendi hii, Liverpool itakuwa nyumbani ndani ya Anfield ikipambana na Arsenal ukiwa ni mwendelezo wa Ligi Kuu England.

Klopp amesema hayo, baada ya kushuhudia juzi Jumanne kikosi chake kikitoka suluhu na Chelsea katika mchezo wa Premier uliopigwa Stamford Bridge.

Arsenal ambao wako moto, watakuwa na kazi ya kupambana na Liverpool ambayo imekuwa haina kiwango cha mwendelezo msimu huu.

Liverpool katika mechi mbili zilizopita, imefanikiwa kupata pointi moja pekee mbele Chelsea, huku ikipoteza dhidi ya Manchester City.

Lakini Klopp anaamini kuwa kiwango walichoonesha wachezaji wake pale Stamford Bridge kitaendelea kuwa bora Anfield  wakatakapovaana na Arsenal.

Klopp ambaye aliipa Liverpool ubingwa wa ligi msimu wa 2019/20 baada ya kupita takribani miaka 30, alisema: “Arsenal wapo juu na wanachez soka safi, lakini naweza kucheza na kuwa bora zaidi yao.

“Mechi ijayo ni dhidi ya Arsenal. Sijui kabisa Arsenal walikuwa nafasi ipi msimu uliopita,  ila kwa sasa wapo juu na wapo vizuri, wanacheza soka zuri ambalo linavutia kuangalia.

“Lakini sasa tutakuwa nyumbani na tukiwa nyumbani  tuna rekodi zetu ndiyo maana tumewekeza nguvu katika mchezo huu.

“Anfield inatusubiri sisi na sisi tunataka kuonesha kitu. Tuna mechi 10 za kucheza na ijayo ni dhidi ya Arsenal, kwa sasa tunawaangalia hawa kwanza.

“Najua kuna ugumu lakini ni lazima tupambane kushinda hii mechi tofauti na hapo watazidi kuwa juu, tunataka kubadili mambo na si vinginevyo.”

MVUTANO WAZUKA BUNGENI, MBUNGE KUCHAUKA na SPIKA TULIA KUHUSU BWAWA LA NYERERE – ”USITUTUME”…

Leave A Reply