The House of Favourite Newspapers
gunners X

Kocha wa Liverpool Afiwa na Mama Yake Mzazi

0

KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp amepata pigo baada ya kufiwa na mama yake mzazi, Elisabeth aliyefariki leo Jumatano, februari 10, 2021.

Klopp hataweza kuhudhuria mazishi ya mama yake nchini Ujerumani, kutokana na masharti makali yaliyowekwa na Ujerumani katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Covid 19.

“Alikuwa ndiyo kila kitu kwangu, alikuwa mama bora sana kwangu, kwa kuwa mimi ni Mkristo, naamini atakuwa sehemu bora peponi, ” amenukuliwa Klopp na kuongeza kwamba maambukizi ya Corona yatakapotulia, amepanga kufanya hafla ya kipekee kumuenzi mama yake huyo.

Elisabeth na mumewe Norbert Klopp aliyefariki mwaka 2000 akiwa na umri wa miaka 66, walifanikiwa kupata watoto watatu, Stefanie, Isolde na Jurgen (Klopp).

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa Twitter, Klabu ya Liverpool imetoa salamu za rambirambi kwa kocha huyo kwa kumsindikiza na maneno ‘You will never walk alone Klopp’ na kusindikizia na alama ya kopa, ukiwa na maana kwamba Klopp hayupo peke yake katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mama yake.

Leave A Reply