The House of Favourite Newspapers
gunners X

Kocha wa Simba Awataka Mashabiki wa Klabu Hiyo Kuwa Watulivu

0
Zoran Maki, Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba

BAADA ya kupoteza mechi kwenye ngao ya jamii dhidi ya Yanga kwa kufungwa bao 2 kwa 1, Kocha mkuu wa klabu ya simba Mserbia Zoran Manojlović Maki amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuwa na utulivu maana wamejiandaa vizuri zaidi kuanza mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold.

 

Kocha huyo amesema wachezaji wote wapo vizuri na wamejiandaa vya kutosha japo ni muda mfupi tangu walipotoka kwenye mechi ya ngao ya jamii.

Zoran Maki

“Ni ngumu kwenda kuanza ligi muda mfupi baada ya kutoka kucheza mchezo mgumu wa ngao ya jamii dhidi ya yanga wachezaji wamejitahidi kurudi katika morali yao ya kawaida.

 

Naye mchezaji shomari Kapombe amewataka mashabiki kuungana na kuisapoti timu yao ili iweze kufanya vizuri zaidi katika kuwania ubingwa wa ligi kuu.

 

Imeandikwa: Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa Mitandao.

Leave A Reply