The House of Favourite Newspapers
gunners X

Majibizano ya Meek Mill na Ex Wake Nicki Minaj (VIDEO)

 

BAADA ya wawili hawa kuachana muda mrefu,  kumekuwa na maneno yanayoendelea chinichini baina yao kupitia vyombo vya habari na kwenye matamasha.

 

Nicki Minaj akiwa katika tamasha lake la muziki huko Australia, aliimba wimbo wa Barbie Dreamz ambao una maneno yanayomsema Meek Mill ambayo aliyatilia mkazo baada ya kumwambia DJ astopishe muziki na kuimba bila sauti ya muziki nyuma.

 

Mstari ambao unamsema Meek kwenye wimbo huo ni , “Meek still be in my DMs, I be having to duck him” aliendelea kukazia akisema, “Ningewaeleza siri lakini sitaki

 

 

 

Kwa upande wa Ex wake Meek Mill aliandika maneno kwenye akaunti yake ya tweeter ambayo yalisemekana kwamba yanakwenda kwa Nicki baada ya kufanya tamasha hilo.

 

Meek aliandika, “Kwa nini unanikasirikia mimi na si watu ambao wanakujia wewe?  Mi nipo poa nafanya vizuri, kuna kitu hakipo sawa hapa.

Tweeter nyingine alikuwa akilalamika aachwe peke yake.

 

 

Wawili hao mahusiano yao yalivunjika Januari 2017 lakini Desemba 2018 Meek alisema kwamba aligundua Nicki amem-block kwenye Instagram wakati alipokuwa anataka kumwangalia kwenye akaunti yake hiyo.

Comments are closed.