The House of Favourite Newspapers
gunners X

Majimaji Yalamba Sh Milioni 150 za Udhamini Kutoka Sokabet

0

Mwenyekiti wa Klabu ya Majimaji, Steven Ngonyani (kulia) na Mratibu wa Sokabet, Franco Ruhinda wakisaini mkataba wa kuidhamini Majimaji.
KAMPUNI ya Mchezo wa Kubashiri ya Sokabet, imezinduliwa rasmi leo Jumatatu, Septemba 4, 2017 katika Hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Oxygen 8 ambao ni wabia wa Sokabet, Shane Leahy, akisaini mkataba huo.

Katika hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wanasoka wa zamani pamoja na waandishi wa habari, ilishuhudiwa kampuni hiyo ikiingia mkataba wa mwaka mmoja na timu ya Majimaji ya Songea, wenye thamani ya Sh milioni 150.

Ruhinda na Ngonyani wakibadilishan mkata huo.
 
Mratibu wa Sokabet, Franco Ruhinda amesema: “Tunayo furaha kuona leo hii tunazindua rasmi Sokabet ambayo itawapa fursa wadau wa kubeti kujishindia mamilioni kwa dau dogo tu watakaloweka kwenye kubashiri kwao michezo mbalimbali ikiwemo soka na ngumi.
 
Ruhinda akimkabidhi jezi yenye nembo ya Sokabet mchezaji wa Majimaji, Jerryson Tegete.

 

 “Lakini pia tunayo furaha zaidi kuingia mkataba na Majimaji ambapo kupitia timu hii inayoshiriki Ligi Kuu Bara, Sokabet itatangazwa kila kona na kujulikana zaidi nchi nzima.”
Ngonyani akifunguka udhamini wa Sokabet kwa Majimaji.

 

Naye mwenyekiti wa Majimaji FC, Steven Ngonyani alisema: “Tunashukuru udhamini huu wa Sokabet kwani utatuongezea kitu kwenye timu yetu hususan katika kujiendesha msimu mzima huu wa ligi ambao una mambo mengi, lakini pia tutaitangaza popote tuendapo.”
 
Aidha, Franco aliongeza kuwa kampuni hiyo ya Kitanzania inaanza ikiwa na mikakati mingi ya kusaidia jamii kwa kile ambacho kitakuwa kikipatikana kutokana na kubashiri, ambapo washiriki wanaweza kujiunga kwa kuingia katika tovuti ya www.sokabet.co.tz.
 

 
Viongozi wa Sokabet wakiwa pamoja na viongozi na wachezaji wa Majimaji.

 PICHA NA AMANI MADEBE | GPL

===

Kumbuka kuwa ili kujiunga na kubashiri ili kuvuna fedha unatakiwa kutembelea tovuti ya www.sokabet.co.tz ambapo humo ndani una nafasi ya kushinda hadi shilingi milioni 100 kwa kuweka Sh 1,000 tu.

SHUHUDIA UZINDUZI HUO.

 

 

 

Leave A Reply