The House of Favourite Newspapers
gunners X

Marekani Yasitisha Viza kwa Raia wa Tanzania Kuanzia Januari 1, 2026

0

Serikali ya Marekani imetangaza kusitisha utoaji wa aina mbalimbali za Viza kwa Raia wa Tanzania kuanzia tarehe 1 Januari 2026, kufuatia Tamko la Rais wa Marekani Na. 10998. ambapo hatua hiyo inahusisha Viza za kutembelea zisizo za uhamiaji pamoja na Viza za masomo na uhamiaji.

Kwa mujibu wa tamko hilo, viza zilizosimamishwa ni pamoja na Viza za kutembelea za Makundi B-1/B-2, viza za Wanafunzi na programu za mabadilishano za Makundi F, M na J, pamoja na Viza zote za uhamiaji, isipokuwa katika hali na mazingira machache yaliyobainishwa.

Makundi yaliyoachwa kwenye usitishaji huo ni pamoja na Viza za uhamiaji kwa makundi maalumu ya kikabila na kidini yanayokabiliwa na mateso nchini Iran, Raia wenye uraia pacha wanaoomba kwa kutumia pasipoti ya Nchi ambayo haijawekwa chini ya usitishaji, pamoja na Viza Maalum za Uhamiaji (SIV) kwa Wafanyakazi wa Serikali ya Marekani kwa mujibu wa Kifungu 8 U.S.C. 1101(a)(27)(D).

Vilevile, Washiriki wa baadhi ya mashindano makubwa ya michezo, pamoja na Wakaazi Halali wa Kudumu wa Marekani (LPRs), hawataathiriwa na usitishaji huo.

Tamko hilo linaeleza kuwa hakuna Viza zilizotolewa kabla ya tarehe 1 Januari 2026, saa 12:01 asubuhi kwa saa za EST, ambazo zimefutwa au zitafutwa kutokana na uamuzi huo hata hivyo, Raia wa Tanzania bado wanaruhusiwa kuendelea kuwasilisha maombi ya Viza na kupanga miadi ya usaili, ingawa wanaweza kukosa sifa za kupewa viza au kuruhusiwa kuingia Marekani.

Leave A Reply