The House of Favourite Newspapers

Matukio Mbalimbali Kutoka Katika Mkutano mkuu wa CCM Taifa Leo – Picha

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dkt. Emmanuel Nchimbi akitoa neno fupi la ukaribisho katika Mkutano mkuu wa CCM Taifa Leo Tarehe 29 Mei 2025.
Wajumbe na waalikwa wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa wakishiriki na kufuatilia Mkutano Mkuu wa CCM Taifa leo Tarehe 29 Mei 2025 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na kufurahia jambo na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi katika Mkutano mkuu wa CCM Taifa Leo Tarehe 29 Mei 2025

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan, amesema marekebisho ya Katiba ya chama hicho yanayopendekezwa ni muhimu ili kukijenga upya CCM kwa kuzingatia mahitaji ya sasa na kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi zake.

Akizungumza katika Mkutano Maalum wa CCM unaoendelea jijini Dodoma, Rais Samia alisema mabadiliko hayo nipamoja na kuongeza mjumbe wa baraza la wadhamini kwa mujibu ya sheria ya vyama vya siasa nchini.

Comments are closed.