The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mavugo: Nikija tu Simba mtafurahi wenyewe

0

mavugo-agiye-kugaruka-muri-kiyovu-_53f3764f70777Straika Laudit Mavugo.

HUKU kukiwa na sintofahamu ya ujio wa straika Laudit Mavugo katika kikosi cha Simba, mchezaji huyo raia wa Burundi amesisitiza kuwa anakuja Tanzania kwa kazi moja tu, kuwafurahisha mashabiki wa Simba. Mavugo ilikuwa asajiliwe na Simba tangu msimu uliopita lakini uongozi wa timu hiyo haukuwa umefi kia makubaliano na wenzao wa Vital’O ambayo straika huyo alikuwa na mkataba nayo.

 

Mavugo ameliambia Championi Jumamosi kutoka Burundi kuwa, anasubiria viongozi wa Simba wamtumie tiketi ya ndege aje Tanzania kufanya vitu vyake katika Ligi Kuu Bara ikiwemo kuifunga Yanga. Simba ilimpa Mavugo Sh milioni 36 kabla ya kuanza msimu uliopita ikiamini ni mchezaji huru, lakini Vital’O walikuja juu na kutaka nao wapewe fedha za kumuuza, lakini mambo yakashindikana.

 

Straika huyo ilibidi akubaliane na Simba kuwa ajiunge na timu hiyo msimu huu ambapo amemaliza mkataba wake na Vital’O. “Nakuja Simba Mungu akipenda kwa sababu mpaka sasa mazungumzo yetu yamefi kia pazuri, kilichobaki nadhani ni wao kunitumia tiketi kwa ajili ya kuja kumaliza baadhi ya mambo ya usajili. “Siwezi kuahidi mambo mengi lakini ambalo nina uwezo nalo ni kufunga, nitahakikisha nazifunga timu tutakazokutana nazo katika michuano yote, nasubiri tiketi na nikija mashabiki watafurahi,” alisema.

 

Moja kati ya timu atakazopambana nazo Mavugo ni Yanga ambayo ina mkali mwingine wa mabao kutoka Burundi, Amissi Tambwe ambaye ni mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita akiwa amefunga mabao 21. Alipotafutwa Rais wa Simba, Evans Aveva alisema: “Kuhusu Mavugo nashindwa kuelewa, kwani hatumpati katika simu yake hivyo tunashindwa kumtumia tiketi, ila kila kitu kipo sawa kwa upande wetu.”

Leave A Reply