The House of Favourite Newspapers

Gamondi kiroho kwatu, awasubiria CR Belouizdad kwa Mkapa

0
Miguel Gamondi

KOCHA Mkuu wa Yanga Muargentina, Miguel Gamondi amefurahishwa na mabadiliko ya viwango va wachezaji wake kuanzia mchezo wa Ligi Kuu Bara walioucheza dhidi ya KMC FC, hali inayompa matumaini ya kupata matokeo mazuri watakapovaana dhidi ya CR Belouizdad ya nchini Algeria.
Timu hizo zinatarajiwa kuvaana Jumamosi hii saa moja kamili usiku, kwenye Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam katika mchezo wa marudiano wa hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katika mchezo wa awali uliochezwa huko Algeria, Yanga alichezea kichapo cha mabao 3-0, ambacho wamepanga kulipa watakaporudiana Jumamosi hii.


Akizungumza na Gazeti la Championi, Gamondi alisema kuwa amefuraishwa na muunganiko wa wachezaji wake aliouona katika mchezo dhidi ya KMC, hiyo imempa matumaini ya kupata matokeo mazuri ya ushindi atakapokuweo nyumbani.
Gamondi alisema mapumziko ya Afcon, yalimvurugia mipango yake kutokana na timu yake kutocheza michezo ya mashndano, na kusababisha muunganiko na mechi fitinesi kupotea.
Aliongeza kuwa amewataka viongozi wake kuendelea kucheza michezo ya Ligi Kuu Bara na Kombe la FA, na kutosimama kuacha viporo kwa lengo la wachezaji wake kutopoteza muunganiko.
“Timu inapokaa muda mrefu bila ya kucheza mchezo wa mashindano, hali ya uchezaji (Rhythm) ya uchezaji pia muunganiko na mechi fitinesi inapotea kwa wachezaji.
“Kabla ya mchezo wa ligi dhidi ya KMC, timu haukucheza vizuri katika michezo yetu mitatu, hiyo ni kutokana na kukaa muda mrefu bila ya kucheza mchezo wa mashindano, lakini baada ya kucheza mechi hizo nimeonma mabadiliko ya wachezaji wangu kucheza kitimu, hiyo imenipa matumaini ya kupata matokeo mazuri dhidi ya Belouizdad,” alisema Gamondi.

STORI NA WILBERT MOLANDI

Gazeti lako bora la Championi linalotoka mtaani mara mbili kwa wiki, Jumatatu na Ijumaa, sasa limekuja kivingine.

Tunatoa zawadi kwako ewe msomaji ambapo kwa kununua GAZETI LA CHAMPIONI, utapata fursa ya kuzawadiwa jezi mpya za Simba na Yanga za msimu wa 2023/2024.

Gusa link hii kusoma Gazeti la Championi leo Jumatatu Feburuari 19, 2024 kila siku kupitia link hii sasa
👇👇👇👇
https://globalapp.co.tz

Leave A Reply