Mazishi ya Jenista Mhagama Kufanyika Desemba 16, Mbinga

Aliyewahi kuwa Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Peramiho, Jenista Joakim Mhagama, aliyefariki dunia tarehe 11 Desemba 2025 jijini Dodoma, anatarajiwa kuzikwa tarehe 16 Desemba 2025, Ruanda – Mbinga.
Ratiba ya Msiba hadi Siku ya Mazishi
DESEMBA 12, 2025
-
Mwili wa Marehemu utaletwa nyumbani kwake Itega, Dodoma kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho.
DESEMBA 13, 2025
-
Misa Takatifu itafanyika katika Parokia ya Kiwanja cha Ndege, Dodoma.
-
Baada ya misa, mwili utasafirishwa kuelekea Songea.
DESEMBA 14, 2025
-
Kuwasili Songea.
-
Maombolezo yataendelea, ikifuatiwa na Misa na mwili kupumzika nyumbani kwake Makambi.
DESEMBA 15, 2025
-
Safari ya kuelekea Peramiho.
-
Misa Takatifu, kutoa heshima za mwisho, na mwili kulala Peramiho.
DESEMBA 16, 2025
-
Mazishi yatakayofanyika Ruanda, Mbinga.


