Meek Mill Kutoa Album Baada Ya Kutoka Jela

RAPA Meek Mill toka Philadelphia ametangaza kutoa albam yake ya kwanza tangu atoke gerezani Aprili mwaka huu ambayo itaongelea masuala mengi yakiwemo yale alipokuwa jela.
Albam mpya ya Meek ambayo haijapewa jina mpaka sasa, itaingia sokoni Novemba 30 mwaka huu. Kwa mujibu wa jarida la Vogue, albam hiyo itakuwa inaongelea haki za kijamii na muda alipokuwa jela.
Taarifa zinasema Cardi B ni mmoja wa wanamuzii watakaopewa shavu kwenye albam hiyo ambayo haina jina mpaka wakati huu na tracklist bado hazijatoka.
Toleo la mwisho la Meek ni Legend Of The Summer EP ambayo ilitoka Julai mwaka huu na ikafanikiwa kushika nafasi ya tisa kwenye Chart za Billboard 200 kwa wiki ya kwanza.


Comments are closed.