The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mke Aliyeuawa Uingereza, Mwili Watua Bongo

MWILI wa Mtanzania, Leyla Mtumwa anayedaiwa kuuawa kwa kuchomwa visu na mumewe, Kema Kasambula, mwezi uliopita unatarajiwa kutua nchini leo baada ya kuagwa jijini London, Uingereza, wikiendi iliyopita.

 

Mwili huo wa Leyla ulikuwa ukishikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Uingereza kwa ajili ya uchunguzi zaidi na baada ya kujiridhisha ndipo wakaukabidhi kwa familia.

Kwa mujibu wa kaka wa marehemu Leyla, Abdulmalick Mtumwa, mwili huo utatua leo jijini Arusha na mara tu baada ya kutua zitafanyika taratibu za kuupumzisha kesho. Leyla anadaiwa kuuawa na mumewe huyo, usiku wa kuamkia Machi 30, mwaka huu jijini humo ambapo sasa jamaa huyo anakabiliwa na kesi ya mauaji.

 

Leyla ni mtoto wa Hidaya aliyeimbwa na Pepe Kalle kwenye wimbo wake wa Hidaya miaka ya 1990, mwenye makazi yake Kaloleni jijini Arusha ambako ndiko msiba ulipo.

 

Stori: Mwandishi Wetu, Dar

Comments are closed.