Mke wa Saidi Fella Awaomba Watanzania na Rais Samia Kumsaidia mume wake – Video

Mke wa Saidi Fella, Sweet Fella, amewaomba Watanzania wajitokeze kumsaidia mume wake ili aweze kurejeshwa India kwa ajili ya matibabu zaidi, akisema hali yake bado inahitaji uangalizi wa karibu.
Akiendelea kuelezea hali ya mumewe, Sweet amesema kuwa kuugua kwa Saidi Fella kwake ni ibada, na kwamba yupo pamoja naye bega kwa bega hadi dakika za mwisho. Ameeleza kuwa leo hii watu wengi hawamuulizii hali mume wake licha ya yote aliyowahi kuwafanyia, lakini yeye anaelewa yote na anaamini Mungu anaona.

Sweet ameongeza kuwa anawatambua wachache wanaojitokeza kuwasaidia katika kipindi hiki kigumu na kuwaombea kwa Mungu awalipe kwa mema yao. Amesisitiza kuwa ataendelea kupambana na watu wanaomsapoti, huku akiahidi kuja kuwashukuru na kuwataja kwa majina baadaye na kumuomba Rais Samia amsaidie kwa anayoyapitia mume wake
Kwa Watanzania walioguswa na hali hiyo na wanaotamani kusaidia gharama za matibabu na safari ya India, mchango wowote unaweza kutumwa kupitia namba 0713781414.
🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like na comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari za kweli na uhakika.

