Mkurugenzi wa FBI Awataka Watu Kutoombeleza Kifo cha Mama Mlezi wa Tupac

Mkurugenzi wa FBI, Kash Patel, ametoa kauli tata akiwataka watu kutoombeleza kifo cha Assata Shakur, mama mlezi wa Tupac
Assata Shakur, ambaye pia alijulikana kama Joanne Chesimard, aliefariki Alhamisi, Septemba 25, 2025, akiwa na miaka 78 mjini Havana, Cuba.
Kifo chake kinasemekana kuwa ni kutokana na matatizo ya kiafya na umri mkubwa.
Patel alimtaja Assata kama gaidi, akiwakumbusha watu hukumu yake kwa kifo cha Afisa wa Polisi wa Jimbo la New Jersey, Werner Foerster, mwaka 1977.
Alihukumiwa kwa mauaji ya daraja la kwanza mwaka huo huo, kisha alikimbia gerezani mwaka 1979 na kupata hifadhi Cuba, ambako aliishi hadi kifo chake mwaka 2025.

Patel alisema: “Kumuombeleza ni kumsaliti afisi na damu ya kila polisi aliyetoa maisha yake kwa huduma.”
Kauli hii imeibua mjadala mkali, kwani baadhi ya watu wanamuona Assata kama shujaa wa kisiasa, huku wengine wakiiona kama hatari. Tukio hili linaonyesha historia changamano ya uhusiano kati ya polisi, haki za kiraia, na harakati za kisiasa nchini Marekani.