Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Atangaza Nafasi za Kazi 23
Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya mwaka 2023/2024 chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 na Kibali cha Ajira mbadala chenye Kumb. Na. FA.228/613/01/C/042 cha tarehe 21 Mei, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro anatangaza nafasi za kazi na anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi za kazi zifuatazo: –