Mnyika: Heche Yupo Kituo Cha Polisi Dodoma
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika amesema ufuatiliaji wao umewezesha kugundua kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, John Heche yupo kwenye Kituo cha Polisi Dodoma.
Mnyika amezitaka mamlaka zinazohusika, likiwemo Jeshi la Polisi na Jeshi la Uhamiaji, kutoa taarifa rasmi kwa umma kueleza mahali alipo na hali yake.
