Mo Dewji: Chama na Luis Miquissone Hawauzwi Popote
BAADA ya kuliibuka na tetesi za Yanga kumnyatia kiungo wa Simba, Cletous Chama na Luis Miquissone ambapo leo Agosti 20, 2020 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ amesema nyota hao hawauzwi popote.
Mo Dewji ameyasema hayo wakati akihojiwa na kituo cha habari cha Wasafi kuwa hivi sasa wanajenga timu yao hakuna fikra yoyote ya kuuza mchezaji wa maana katika kikosi chao.
Kuhusu kujiuzulu kwa aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa, amesema kuwa walimweleza mtendaji huyo kupunguza matumizi na kuongeza mapato lakini wakiwa wanaingia katika kikao cha bodi ili kumjadili kwa muda aliofanya kazi aliamua kujiuzulu.
“Senzo inasemekana ameondoka na nyaraka za klabu ameenda kuwapa wenzetu, wala hatuna wasiwasi wowote katika hilo kwani siku si nyingi tutamtangaza Ofisa Mtendaji mkuu mpya,” amesema Mo Dewji Kuelekea siku ya kilele cha Simba Day, Ofisa habari wa Simba Haji Manara amesema wamepanga kupata watu 100,000 watakaokuwa uwanja wa Mkapa, Uhuru na nje ya uwanja.
“Nilikuwa sipo sawa kiafya ndio maana niliandika kuachia nafasi hii kutokana na kuchoka lakini baada ya kwenda hospitali niliambiwa nipo fiti kwa maana hiyo naendelea na majukumu yangu ya kila siku kama kawaida,” amesema Manara.





